Tuesday, July 16, 2013

HARVARD UNIVERSITY yampatia shavu la heshima NAS!!


Mkongwe katika muziki wa HIP HOP kutoka marekani almaarufu kama NAS ambae ni mtu muhimu kwa muziki wa HIP HOP alitikisa anga kwa takriban miongo miwili sasa na kuweza kujipatia multiplatinum huku akiwa chini ya kampuni kubwa ya utayarishaji  muziki ya Def Jam Records amepewa shavu hilo la kuandaliwa fellowship yake itakayojulikana kwa jina la NASIR JONES FELLOWSHIP yenye lengo la kusaidia vijana ambao wanataaluma ya muziki na utamaduni wa HIP HOP kuweza kupata mafunzo ya muziki huo sambmba na scholarship ilikuweza kujiendeleza kimasomo zaidi

Akiongea kuhusina na ujio huo Prof  Henry Louis Gates, Jr ambae ni mkurugenzi wa   W. E. B.DU Bois Institute for African and African American Research alisema kuwa wameamua kumtumia NAS kwa kuwa anamuonekano ambao unaweza kuwasaidia vijana  kujifunza na kuweza kufanikisha kile wanachotaka kufanya ili kufikia malengo yao katika sanaa na taaluma zao

NAS amabeo ameweza kujipatia umaarufu mkubwa hapa ulimwenguni kwa kuweza kuwa ni mmoja kati ya ya ma MC wachache wenye utaalamu mkubwa wa kupanga na kutengeneza mashahiri yenye kutoa ujumbe mzito na kuelimisha sana jamii na kukosoa pale anapoona ukoswaj katika maswala yanayowahusu wanajamii. hii ndio nafasi yake sasa kulipwa fadhila zake alitanabaisha Prof Henry Louis Gates Jr kutoka HARVARD UNIVERSITY

No comments: